Home » Mchungaji Ezekiel Apata Ushindi Kortini

Hakimu Benmark Ekhubi ameamuru idara Upelelezi wa makosa ya Jinai (DCI) kukamilisha uchunguzi wao dhidi ya Mchungaji wa Kanisa la New Life International Ezekiel Oder ndani ya siku 14.

 

Kupitia Mawakili wake, Mchungaji Ezekiel aliomba siku za uchunguzi wa tuhuma za utakatishaji fedha zipunguzwe kutoka 30 hadi 15 ili kuharakisha shughuli zake za Kanisa.

 

Kwa hivyo, akaunti za benki za Odero zitafungiwa kwa siku 14, maagizo yakiisha Jumapili, Mei 21.

 

Katika uamuzi huo Ekhubi, amedai wahusika wote kufika mahakamani Jumatatu Mei 22, kesi hiyo itakapotajwa kwa maelekezo na maagizo zaidi.

 

Kuhusu iwapo mahakama ilifuata vifungu vya kisheria vya kufungia akaunti za Mchungaji Ezekiel, Hakimu Ekhubi ameeleza kuwa Sheria ilimruhusu kutoa amri hizo kwa polisi.

 

Hii ilikuwa baada ya Wakili Danstan Omari, aliyemwakilisha Mchungaji Ezekiel, kulalamika kwamba polisi waliidanganya mahakama kutoa maagizo hayo.

 

Hakimu Ekhubi pia ametupilia mbali pingamizi la awali ambapo Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (ODPP) ilipinga ombi la Mchungaji Ezekiel.

 

Upande wa Mashtaka ulidai kuwa maafisa kutoka Idara ya (DCI) walihitaji muda zaidi kukagua ushahidi huo.

 

Hakimu pia atatoa uamuzi katika ombi ambalo Mchungaji Ezekiel alitaka aruhusiwe kupata baadhi ya akaunti zake za benki hata uchunguzi ukiendelea.

 

Mnamo Jumanne, Mei 16, Mchungaji Ezekiel alielekea kortini akimwomba Hakimu amruhusu kukusanya hadi Ksh50 milioni kutoka kwa akaunti hizo.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!