Home » Maafisa 6 Wa Polisi Washambuliwa Na Wachuma Chai Bomet

Maafisa 6 Wa Polisi Washambuliwa Na Wachuma Chai Bomet

Maafisa sita wa polisi walio katika kituo cha polisi cha Konoin kaunti ya Bomet wanaendelea na matibabu katika hospitali ya rufaa ya Kaunti ya Kericho kufuatia shambulio la wachumaji chai katika shamba la chai huko Bomet Jumapili jioni.

 

Kulingana na kamanda wa polisi wa Kaunti ya Bomet Mathews Mangira, maafisa wawili waliojeruhiwa wako katika hali mbaya wakiwa na majeraha mengi kwenye miili yao.

 

Wakati wa kisa hicho, afisa mwingine aliyejaribu kubadilisha njia yake ya kurudi kituoni kwa miguu baada ya kupotea katika Mto Itare alikabiliwa na watu hao wengi wao wakiwa vijana ambao kulingana naye walimpora baadhi ya silaha alizokuwa nazo na kumuacha katika hali mbaya baada ya kumvamia.

 

Mangira anasema maafisa hao walikuwa kwenye doria yao ya kawaida ndani ya shamba la chai kabla ya kukutana na zaidi ya vijana 100 waliokuwa na silaha hatari ambao walikabiliana nao wakiwa na nia ya kuvuka hadi kwenye shamba la kibinafsi la chai la Finlays.

 

Timu ya maafisa wa DCI wametumwa kuwasaka washukiwa ambao bado hawajakamatwa.

 

Gari lililoharibika lilivutwa hadi kituo cha polisi cha Mara Mara.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!