Home » Ruto Na Raila Wapeana Mikono

Semi na cheche za siasa zimesheheni hafla ya mazishi inayoendelea ya mkewe Dedan Kimathi Mukami Kimathi ambapo maziko hayo yanafanyika Njabini kaunti ya Nyandarua.

 

Rais William Ruto awali na Kiongozi wa Azimio Raila Odinga walipeana mikono baada ya miezi kadhaa ya mzozo wa kisiasa.

 

Odinga alifika kwenye mazishi hayo eneo la Njabini, Kaunti ya Nyandarua akiandamana na aliyekuwa mbunge wa eneo hilo Jeremiah Kioni na aliyekuwa Gavana wa Kaunti ya Muranga Mwangi wa Iria.

 

Mukami Alifariki Mei 11 katika Hospitali ya Nairobi akiwa na umri wa miaka 101.

 

Mazishi ya mjane huyo wa mpigania uhuru wa Mau Mau Dedan Kimathi yamehudhuriwa na viongozi wakuu akiwemo Naibu Rais Rigathi Gachagua pamoja na viongozi mbalimbali.

 

Odinga aliongoza maandamano mwezi Aprili kupinga gharama ya juu ya maisha na ushindi wa urais anaodai uliibiwa kutoka kwake, jambo lililomfanya rais kuanzisha mazungumzo kupitia Bunge ambapo yanaongozwa na wabunge wa pande zote mbili.

 

Aidha viongozi wengi wamedai kwa sasa yafaa raila Odinga kusitisha maandamanao na kupea serikali ya Kenya kwanza muda wa tekeleza majukumu yake ya kurejesha maisha katika hali ya kawaida.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!