Home » Miili 29 Zaidi Yafukuliwa Shakahola

Zoezi la ufukuaji wa miili limeendelea hii leo katika msitu wa Shakahola kaunti ya Kilifi ambapo miili 29 zaidi imefukuliwa kutoka kwa makaburi 12.

 

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Rhoda Onyancha, katika taarifa kwa vyombo vya habari, amesema idadi ya waliofariki kutokana na mafundisho yanayoongozwa na mchungaji Paul Mackenzie sasa imefikia 179.

 

Onyancha ameongeza kuwa hakuna watu wapya waliokamatwa au kuokolewa wakati wa operesheni hiyo na kudai kuwa watu 15 zaidi pia wameripotiwa kutoweka, na hivyo kufanya idadi hiyo kufikia 609.

 

Haya yanajiri huku Mackenzie na washtakiwa wengine 17, akiwemo mke wake, Jumatano wakizuiliwa kwa siku 30 zaidi wakisubiri kukamilika kwa uchunguzi wa dhehebu la Shakahola.

 

Uamuzi huo ulitolewa na Hakimu Mwandamizi Yusuf Shikanda ambaye alisema kuwaachilia huru washukiwa hao kutahatarisha usalama wao pamoja na upelelezi unaoendelea.

 

Kanisa la Good News International la Mackenzie limepokea notisi za kufungwa kutoka kwa Msajili wa Vyama kwa kutofuata sheria za kidini.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!