Home » Kindiki: Hatuko kwenye Vita Na Dini

Serikali inasisitiza dhamira yake ya kutetea haki ya kikatiba ya uhuru wa kuabudu huku kukiwa na uchunguzi kuhusu shughuli za ibada katika msitu wa Shakahola ambapo zaidi ya miili 109 ilikuliwa.

 

Waziri wa Mambo ya Ndani Kithure Kindiki amepuuzilia mbali madai kwamba serikali inanuia kuanzisha vita dhidi ya taasisi za kidini, akifafanua kwamba lengo kuu limelenga kuwaondoa viongozi wa dini walaghai wanaoendeleza itikadi kali na uhalifu.

 

Kindiki amekariri kuwa serikali haijakatishwa tamaa na kelele za watu ambao wanadai serikali inaenda kinyume,,,,,na itaendelea kulenga kuwawinda wale wanaotumia vibaya ushawishi wa kidini kwa nia potofu,

 

akitaja mkasa wa Shakahola kama ushahidi wa vurugu kubwa na unyanyasaji wa kiroho ambao serikali inataka kuepusha wakenya.
Kulingana na Kindiki, miili 112 imefukuliwa kutoka shakahola huku zoezi la uchimbaji likitarajiwa kuanza kesho Jumanne baada ya kusitishwa kutokana na hali mbaya ya hewa.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!