Home » Davido Aisifu Single Again Ya Harmonize
Davido aisifu Single again ya Harmonize

 

Mwanamuziki nyota kutokea Nigeria Davido aisifu Single Again, ngoma ya nyota kutokea Tanzania Harmonize ambayo pia imeonesha kuota mabawa na kutamba duniani kote..

SOMA PIA: Wizkid Amwonyesha Davido Upendo

Kupitia screenshot ambayo Harmonize aliamua kuweka katika ukurasa wake wa Insta story, ilionesha ya kuwa Davido alimtumia ujumbe kwa kuisifu ngoma hiyo na kueleza ya kuwa pia mkewe Chioma anaipenda sana ngoma hiyo.

 

Ujumbe wa Davido Kwa Harmonize

 

Tangu Davido aisifu Single Again limekuwa jambo la kujivunia kwa msanii huyo baada ya kuona ya kuwa hata wasanii wakubwa wa Afrika kama Davido wameonesha kuzikubali kazi zake mpaka kufikia hatua ya kumtumia ujumbe wa pongezi.

 

Ngoma ya Single Again iliachiliwa mwaka huu wa 2023 na kwa mujibu wa Tembo maudhui ya wimbo huo ulitokana na kitendo cha yeye na aliyekuwa mpenzi wake Kajala kuachana. Kwa maana hiyo Single Again imeelezea chanzo cha anguko la penzi lao.

 

Baada ya Davido kuisifu Single Again pengine tutarajie ukurasa mpya wa Harmonize na wasanii kutokea nje ya nchi kwa maana ya Davido baada ya miaka mingi kupita baada ya kufanikiwa kufanya ngoma na wasanii wa Nigeria kama vile Burna boy, Yemi Alade pamoja na Skales.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!