Home » Mwanafunzi Afariki Maji Homa Bay

Mwanafunzi wa darasa la nne alikufa maji alipokuwa akijaribu kuogelea kwenye maji katika kijiji cha Rapedhi huko Ndhiwa, Kaunti ya Homa Bay, Jumanne jioni.

 

Mvulana huyo mwenye umri wa miaka 14 alikuwa pamoja na kaka yake wakati wote wawili waliamua kuogelea kwenye maji hayo.

 

Kulingana na chifu msaidizi wa eneo hilo, Neto Akech, watoto hao walijaribu kutumia gome la mmea wa migomba kujaribu kuvuka kutoka upande mmoja hadi kwingine walipokuwa wakiogelea lakini marehemu alipofika katikati, alishindwa na kudhibitiwana maji yaliokuwa yakienda kwa kasi.

 

Kaka yake alikimbia kurudi nyumbani kumjulisha baba yao, lakini wenyeji waliofika eneo la tukio walifanikiwa kuuchukua mwili huo na kuhamishiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Manyatta Kobodo.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!