Home » Gachagua Ampiga Samidoh Marufuku

Naibu Rais Rigathi Gachagua amefichua sababu iliyomfanya katika miezi ya hivi majuzi msanii wa Mugithi ambaye pia ni afisa wa polisi Samidoh kutofanya ziara yake ya kimuziki nje ya nchi.

 

Akizungumza kwenye sherehe ya miaka 25 ya safari ya muziki ya mwanamuziki mkongwe Muigai wa Njoroge wikendi, naibu rais Gachagua alisema kuwa alitambua kwamba Samidah alihitaji kuleta utulivu kwa wake zake wawili, Edday Nderitu na Karen Nyamu.

 

Gachagua alifichua kuwa alihakikisha kuwa Samidoh amepigwa marufuku kusafiri nje ya nchi ili kusuluhisha tofauti kati ya Nyamu na Nderitu.

 

Hata hivyo, Gachagua alisema kuwa marufuku hayo huenda yakaondolewa kwa sababu alisema kuwa msanii huyo amefaulu kwa kiasi kikubwa kuleta mwafaka kati ya Nyamu na Nderitu.

 

“Nilikuwa nimemzuia Samidoh kwenda nje ya nchi lakini sasa nimemruhusu kwenda kufanya shoo huko kwa vile ameiweka sawa nyumba yake Sasa kuna amani na heshima fulani. Samidoh pia ni polisi wetu. Ataruhusiwa kwenda lakini hatakiwi kuwaambia wazungu siri zetu.”

 

Aidha, hii si mara ya kwanza kwa Gachagua kumweka Samidoh wazi kuhusu mahusiano yake. Mnamo Januari mwaka huu, Gachagua aliwasha moto kuhusiana na jinsi Samidoh alivyowashughulikia wapenzi wake, akisema alihitaji kuwadhibiti wanawake wake dhidi ya kusababisha drama nyingi.

 

“Samidoh dhibiti watu wako. Dhibiti watu wako na ukishindwa tutakupiga marufuku kusafiri nje ya nchi,” alisema.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!