Home » Diamond Awapiku Burna Boy, Wizkid YouTube

 

Kwa ukanda wa Afrika Mashariki moja kati ya wasanii ambao  ni wakujivunia ni pamoja na Mkurugenzi wa WCB Wasafi Diamond Platnumz. Jambo hili limethibitika mara baada ya Diamond ameongoza Youtube kwa kuwa na watazamaji wengi mjini huko kwa upande wa kusini mwa Jangwa la Sahara.

 

SOMA PIA:Diamond Platnumz Na Shilole Wateuliwa Na Rais Samia

 

Kulingana na Takwimu zilizotolewa na TopChartsAfrika zimemtaja Diamond Platnumz kuwa ndiye msanii anayekimbiza kwa kuwa na watazamaji wengi zaidi Youtube.

 

 

Diamond Platnumz

Kwa mujibu wa takwimu hizo, Diamond ameongoza kwa kuwa na jumla ya watazamaji Bilioni 2.14, akifuatiwa na Burna boy kutokea Nigeria 2.05, Wizkid 1.67, Fally Ipupa 1.40 na huku namba tano ikishikwa na Davido kwa kuwa na jumla ya watazamaji 1.29.

 

Hatua hiyo aliyoipiga Diamond kwa kuwa na watazamaji wengi Youtube ni pamoja na mchango wake ambao umechangiwa na EP yeke ya First Of All ambayo iliiachia mwaka jana ikiwa na nyimbo kama Mtasubiri, Sona, Fine, Wonder pamoja na nyingine nyingi.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!