Home » Agnes Kalekye Achaguliwa Mwenyekiti Wa Chama Cha Wamiliki Wa Vyombo Vya Habari

Agnes Kalekye Achaguliwa Mwenyekiti Wa Chama Cha Wamiliki Wa Vyombo Vya Habari

Afisa Mkuu wa mtendaji wa Radio Africa, Agnes Kalekye amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari nchini Kenya.

 

Aliteuliwa wakati wa mkutano mkuu wa mwaka uliofanyika Ijumaa, 28 Aprili 2023 Anachukua nafasi ya Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Nation Media Group (NMG) Stephen Gitagama ambaye alihudumu kama Mwenyekiti kwa mihula mitatu mfululizo.

 

Kalekye ameahidi kulinda maslahi ya wanachama na kukuza ubora katika uandishi wa habari.

 

Viongozi wengine waliopigiwa kura ni Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Mediamax Group, Ken Ngaruiya Makamu Mwenyekiti, Mkurugenzi Mtendaji wa Kass TV, Julius Lamaon kuwa Katibu wa Heshima, Arjun Ruzaik Mweka Hazina na mkuu wa KBC, Samuel Maina kama Katibu.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!