Home » Neymar Kupata Mtoto Wa Kiume

 

Kipanga wa soka anayekipiga katika klabu ya soka ya Paris Saint Gemain Neymar Da Silva Santos ametangaza ya kuwa yuko mbioni kupata mtoto wake wa kwanza na mchumba wake Bruna Biancardi.

 

Siku ya Jumatano kupitia katika kurasa zao za Instagram, wawili hao walitangaza kupata mtoto huyo huku mimba ikionekana kuwa bado ni changa lakini shauku yao ikiwa ni kubwa zaidi.

 

SOMA PIA:Shilole Ajikita Kuwekeza Katika Ardhi

Taarifa hizo pia zinamweka Neymar Jr katika nafasi ya kuwa baba wa watoto wawili baada ya mtoto wake wa kwanza Davi Lucca mwenye miaka 12 aliyempata na Carolina Dantas.

 

Neymar na Bruna walianza mahusiano mwaka 2021 lakini yalikuwa mahusiano ya siri mpaka ilipofika mwaka 2022 na kuamua kuweka hadharani mahusiano hayo na sasa wakitarajia mtoto wao wa kwanza pamoja.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!