Zaidi Ya Wanafunzi 60,000 wa PP1, PP2 Meru Kunufaika Na Vitabu Vya Thamani Ya KES 10M
Serikali ya kaunti ya Meru imepata shehena ya vifaa vya vitabu ambavyo vina thamani ya zaidi ya Kshilingi milioni 10, ushirikiano kati ya Serikali ya Kaunti ya Meru na shirika la uchapishaji la serikali nchini (KLB).
Zaidi ya vitabu elfu 26,000 vitanufaisha wanafunzi elfu 60,000, ambavyo vinakusudiwa kwa wanafunzi wa PP1 na PP2 katika vituo mia 776 vya ECDE katika kaunti hiyo ambavyo vile vile Vitabu vimeidhinishwa na Taasisi ya Ukuzaji Mitaala ya Kenya (KICD).
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa vitabu hivyo, Gavana wa Meru Kawira Mwangaza amesema kuwa hiyo ni hatua nzuri kwa sababu ina gharama nafuu, na itaboresha pakubwa upatikanaji wa vifaa vya elimu.
Kwa miaka mingi, zaidi ya wanafunzi 7 wamekuwa wakitumia kitabu kimoja katika kaunti hiyo, na mpango huo sasa utawezesha wanafunzi 3 kutumia kitabu kimoja.
Kawira amehakikisha kwamba vitabu hivyo vyote vinawasilishwa kwa shule zitazofaidika kutoka sehemu moja hadi nyingine katika juhudi za pamoja za kukuza shughuli za masomo.