Home » Kenya Yatuma UjumbeWa Dharura Kwa Raia Wake Mjini Khartoum

Kenya Yatuma UjumbeWa Dharura Kwa Raia Wake Mjini Khartoum

Rais William Ruto amehimiza mifumo ya amani kusuluhisha hali inayoendelea nchini Sudan baada ya mapigano makali kuzuka.

 

Katika taarifa yake, rais amezitaka pande zote kuzingatia mazungumzo kwa ajili ya utulivu wa nchi na raia wake.

 

Ruto ameongeza kuwa serikali ya Kenya pamoja na mataifa mengine ya Jumuiya ya Maendeleo ya (IGAD) iko tayari kusaidia katika kufanikisha mapatano kati ya pande hizo mbili na kurejesha amani nchini humo.

 

Serikali ya Kenya, kupitia Wizara ya Mashauri ya Kigeni, iliwashauri Wakenya wote nchini Sudan kuwasiliana kwa haraka na ubalozi wa kenya kusalia majumbani kutokana na machafuko ya Khartoum.

 

Viongozi kadhaa duniani akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken na Moussa Faki Mahamat, mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika wametoa wito wa kukomesha ghasia.

 

Aidha Shirika la ndege la Kenya Airways (KQ) pia lilisitisha safari zote za ndege kwenda na kutoka Khartoum, Sudan hadi ilani nyingine.

 

KQ iliwashauri abiria wake kuwa watafuatilia hali ilivyo na kuwajulisha watakaporejelea huduma zao.

 

Ndege iliyokuwa ikielekea Nairobi ilielekezwa Athens, Ugiriki kufuatia machafuko hayo. Mwakilishi wa shirika hilo la ndege, ambaye alizungumza na vyombo vya habari, alidokeza kuwa uamuzi huo ni wa hatua za usalama.
Ghasia hizo zimeripotiwa kuzuka baada ya Kikosi cha Kusaidia (RSF) kushambulia makazi ya Jenerali wa Jeshi la Sudan Abdel Fattah Al-Burhan na baadae kudai udhibiti wa viwanja vyote vya ndege.

 

Hii ilisababisha ndege kadhaa kuchomwa moto huku shughuli zote katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Khartoum zikisitishwa.
call; +249 900 194 854.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!