Home » Rosa Ree Aja Na Ngoma Ya I’m Not Okay

 

Mwanamuziki Rosa Ree ameachia ngoma yake aliyoipa jina la I’m not Fine zikiwa ni siku chache tu baada ya mwanadada huyo kuweka video katika ukurasa wake wa Instagram ambayo ilimuonesha akiwa analia huku akisema hayuko sawa.

 

SOMA PIA:Rosa Ree Amwaga Machozi, I’m Not Fine

 

Katika ngoma hiyo ya I’m not fine, Rosa Ree ametumia mashahiri yake kujiweka katika nafasi ya kueleza hisia zake kwa ugumu anaopitia na vitu ambavyo huvifanya ili basi tu aweze kujisikia vizuri ikiwemo kunywa pombe.

 

 

Wimbo huo pia mshiriki huyo wa tuzo za TMA ameweza kuufikisha kwa mashabiki zake wote haswa wale wanaopitia vipindi vigumu na kukosa watu wa kuwaeleza jinsi ambavyo wanajisikia.

 

Wengi walitafsi kuwa video ile ilikuwa kwa lengo la kuachika kazi yake ingine na kimekuwa ni kitu cha kweli baada ya wimbo huo kutoka. Lakini pia si mbaya kama mtu akiamua kutumia kipaji chake cha sanaa na kuweka wazi hisia zake ikiwa ni kazi ya sanaa na ubunifu. Zaidi Rosa Ree ameweza kuielezea jamii kubwa ya watu ambao wanakutana na changamoto kama hizo na yeye mwenyewe akiwa mhanga.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!