Home » Mwijaku Amtaka Rayvanny Amuoe Fahyma

Forever Rayvanny X Fahyma

 

Mtangazaji kutokea kituo cha radio cha Clouds FM Mwijaku amemtaka Rayvanny amuoe mama mtoto wake Fahyma mara baada ya kuchora jina lake katika sehemu ya mkono wake.

 

SOMA PIA:Nakupenda Yamuingizia Jay Melody 200M+

 

Povu hilo limemmwagika balozi huyo wa makampuni mbalimbali ambaye amekuwa akiwakosoa mastaa wengi Tanzania kulingana na maoni yake juu ya vitu ambavyo hufanya na mastaa hao haswa katika maisha yao binafsi.

 

Katika kutoa ushauri huo Mwijaku aliandika katika ukurasa wake wa Twitter pamoja na Instagram ya kuwa Kumchora TATTOO si kumheshimisha mwanamke. Muoe umpe heshima na apate baraka kwa Mungu. Umemtesa sana na wasambaza U.T.I sugu.

 

 

Mwijaku amemtaka Rayvanny amuoe Fahma kwa kuwa hiyo ndiyo itakuwa heshima na si kuchora Tattoo yenye jina lake kwa maana ya kuwa nu muda sasa wawili hao wamekuwa katika mahusiano ambayo kuna muda pia yalivunjika na wakarudiana

 

Rayvanny na Fahyma ni wapenzi ambao kwa sasa tayari wameshabarikiwa mtoto mmoja na hivi karibuni wawili hao walishuhudiwa katika video mpya na msanii Rayvanny aliyoipa jina la Forever.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!