Home » Kindiki: Biashara Ya Dawa Za Kulevya Ni Tishio Kuu Kwa Usalama Wa Taifa

Kindiki: Biashara Ya Dawa Za Kulevya Ni Tishio Kuu Kwa Usalama Wa Taifa

Waziri wa Mambo ya Ndani Prof. Kithure Kindiki ameainisha biashara na matumizi mabaya ya pombe haramu na dawa za kulevya miongoni mwa tishio kuu za usalama wa taifa baada ya ugaidi na ujambazi.

 

Akiongea leoh ii Ijumaa, Prof. Kindiki ameahidi kuanzisha vita vikali ili kukabiliana na tishio la pombe haramu na dawa za kulevya ambalo anasema ni tishio kwa mustakabali wa nchi.

 

Kindiki amekuwa akizungumza mjini Nyeri wakati wa kongamano la mashauriano la wadau kuhusu tishio la unywaji pombe haramu na dawa za kulevya nchini.

 

Kongamano hilo limeongozwa na Naibu Rais Rigathi Gachagua.

 

Prof.Kindiki amewataka wadau wote kuungana na kuisaidia serikali katika vita dhidi ya dawa za kulevya na matumizi ya dawa za kulevya.

 

Kongamano hilo liliitishwa katika makazi ya Mratibu wa Kanda ya Nyeri na kuwaleta pamoja Maafisa wa Utawala wa Serikali ya Kitaifa wakiwemo makamishna wa kaunti, machifu, Huduma ya Kitaifa ya Ujasusi, K.R.A, KEBs na viongozi waliochaguliwa miongoni mwao magavana na Wabunge.

 

Kongamano la leo limewaleta pamoja viongozi kutoka kaunti za Mlima Kenya za Nyeri, Kirinyaga, Kiambu, Muranga na Nyandarua.
Kongamano sawia na hilo litafanyika Embu, Nakuru, Wajir na Eldoret.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!