Home » Mwili Wa Daktari Kule Nandi Wapatikana Ukiwa Unaoza Karibu Na Sehemu Za Chemichemi

Mwili Wa Daktari Kule Nandi Wapatikana Ukiwa Unaoza Karibu Na Sehemu Za Chemichemi

Daktari wa Nandi ambaye aliripotiwa kutoweka wiki mbili zilizopita amepatikana akiwa amefariki.

 

Mwili uliokuwa ukioza wa Dkt Caleb Tanui, daktari wa magonjwa ya wanawake, ulipatikana kwenye sehemu zenye chemichemi karibu na Mto Kingwal katika Kaunti ya Nandi wakati wa msako wa maafisa wa polisi.

 

Polisi wanashuku Dkt Tanui alikufa maji alipokuwa akijaribu kuvuka mto huo.

 

Uchunguzi wa baada ya maiti haukupata dalili zozote za kuumia au kunyongwa kwenye mwili wake.

 

Kamanda wa polisi wa kituo cha Nandi Doris Chemosi amesema sampuli zimepelekwa katika maabara kwa uchunguzi zaidi.

 

Mwanafunzi huyo wa zamani wa Shule ya Upili ya Mang’u jamaa wake wanadai alikuwa mtu mahiri na wa kijamii.

 

Hapo awali alifanya kazi katika Kaunti ya Kericho na kuhamishwa hadi Kaunti ya Narok ambako alifanya kazi hadi wakati wa kifo chake.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!