Nandy Amzawidi Mumewe Gari Siku yake ya Kuzaliwa

Mwanamuziki ambaye pia ni mmiliki wa lebo ya African Princess Nandy, amemzawadia mume wake BillNass gari aina ya Range Rover wakati wa kusheherekea siku yake ya kuzaliwa. Siku hiyo ilifanyika Tarehe 11 April ambapo Nenga alikuwa akitimiza miaka 30.
SOMA PIA: Marioo, Paula Wazama Penzini
Gari hilo alilozawidiwa Bilnass limekadiriwa kufikia thamani ya Milioni 200 za kitanzania na pia katika sherehe hizo alipokea fedha mbalimbali kutoka kwa wasanii wenza akiwemo Raynanny
Penzi la wawili hawa lilitaradadi zaidi kwa umma mara baada ya ndoa yao tu kufungwa katika kanisa la KKKT Usharika wa Mbezi Beach na baada ya Nandy kufanikiwa kijifungua.
Wawili hao wamezidi kuonekana wakila bata katika nchi mbalimbali ikiwemo Ufaransa, huku mitandao yao ya kijamii ikipambwa na picha zao na maneno ya mahaba juu yao.
Billy Nass na Nandy kwa sasa ni moja kati ya wanandoa maarufu sana nchini Tanzania mara baada ya kufunga ndoa mwaka uliopita na kwa sasa wakiwa tayari wamebarikiwa na mtoto wao wa kwanza ambaye bado hawajamuweka hadharani.
Katika sherehe hiyo ya siku ya kuzaliwa ya Bill Nass wasanii na mastaa mbalimbali walihuudhuria akiwemo Whozu, Rayvanny, Yammy TZ pamoja na wengine wengi.