Marioo, Paula Wazama Penzini
Nyota wa muziki ambaye kwa sasa bado anatamba na Albumu yake ya The Kid You Know, Marioo amethibitisha penzi lake dhidi ya mrembo Paula Kajala siku za hivi karibuni.
SOMA PIA:Rosa Ree Amwaga Machozi, I’m Not Fine
Mwanamuziki huyo alichapisha picha na mwanadada Paula akiwa anajirekodi na kionjo cha wimbo wa Ananipenda ambao kwa sasa bado hajauachia. Katika video hiyo Marioo aliambatanisha pamoja na ujumbe ulioosema
Imagine Mtoto Mbichi kama huyu afu anakupenda
Sambamba na hilo mrembo huyo pia aliaujibu ujumbe huo kwa kuandika ya kuwa
I wish i met you earlier 🥹❤️🔥
Bila kupitwa na jambo hilo naye mtangazaji wa kituo cha radio cha Wasafi FM, Juma Lokole alichapisha video fupi kupitia ukurasa wake wa Instagram ambayo iliwaonesha wawili hao wakiwa katika mahaba mazito huku wakikumbatiana kwa mahaba mazito.
Ujio wa taarifa za kuwepo kwa mahusiano ya kimapenzi kwa wawili hao ni siku chache tangu msanii Rayvanny alipoachia video yake ya Forever ambayo ilithibitisha kurejea kwa penzi lake na mama watoto wake Fahyma