Mume Amtaliki Mkewe Kwa Kuwagawia Watoto Wa Majirani Chakula
Mahakama nchini Zambia imewataliki wanandoa wa miaka zaidi ya ishirini baada ya mume kukiri mkewe hupika chakula zaidi ya kipimo chake na kuwagawia watoto wa majirani.
Kulingana na ripoti ya Zambian Observer kwenye Tovuti yake, mume, George Phiri, 49 mkaazi wa eneo la Matero, mkewe ana hulka za kupika chakula zaidi ya kipimo ambacho yeye humpa na pia ana mazoea ya kupika chakula nyuma ya uwepo wake.
Akizungumza mbele ya Hakimu Mfawidhi Harriet Mulenga, Phiri aliongezea kuwa tabia za mkewe licha ya kumuonya kwa muda, zimekuwa kero kwake hasa katika hali ngumu ya uchumi ambapo mkewe huwaitia chakula watoto wa majira zake.
Tanta Zulu, 34 mshitakiwa, alijitetea mbele ya mahakama siku ya Ijumaa kwa kusema kwamba mumewe ni bahili na ana mazoea ya kumpimia chakula, kumpiga na pia kumtishia kumwacha iwapo hatifuata masharti anayopewa.
Hakimu Mfawidhi baada ya kuangalia kwa undani kesi ya Phiri, alisema kwamba kesi hiyo haikuwa na mashiko ila kutokana na kusisitizwa kwa talaka, wawili hao( Phiri na Zulu) hawakuwa na budi kutenganishwa.