Home » Ruben Kigame: Ni wakati Wa Viongozi Pia Kuhisi Jinsi Tunavyohisi

Ruben Kigame: Ni wakati Wa Viongozi Pia Kuhisi Jinsi Tunavyohisi

Aliyekuwa mgombea Urais Reuben Kigame amesema kuwa mishahara iliyocheleweshwa ya wafanyikazi wa umma inapaswa kuwa mwanga wa tahadhari kwa viongozi kuhusu haja ya kushughulikia masuala muhimu yanayowakabili Wakenya.

 

Kulingana na Kigame, ucheleweshaji huo sasa utawapa viongozi mtazamo wa moja kwa moja wa wakati mgumu ambao Wakenya wanalazimishwa kuhudumu wakiwa na mishahara ya chini au bila malipo yoyote.

 

Akizungumza leo hii Jumatatu, Kigame amesema kuwa ni wakati mwafaka wa viongozi kuelekeza nguvu zao kushughulikia masuala yanayowasumbua Wakenya na kujiepusha na “siasa nyingi”, akisema kwamba wanapaswa kutimiza ahadi zao za kampeni.

 

Haya yanatokana na hisia za Naibu Rais Rigathi Gachagua, ambapo alikiri kuwa serikali inakabiliwa na changamoto za kifedha, na kulemaza malipo ya mishahara.

 

Naibu rais Gachagua aliongeza kuwa baadhi ya mikopo ya serikali ilikuwa inaisha uda wake wiki jana, na kuilazimu kulipa deni hilo.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!