Home » Diamond, Mabantu Kudondosha Kolabo

 

Bosi na mmiliki wa lebo ya WCB Wasafi Diamond Platnumz ametangaza kutoa kazi zake mbili alizowashirikisha Mabantu mara baada ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani kumalizika.

 

SOMA PIA:Diamond Platnumz Kuwekeza Katika Sekta Ya Anga Tanzania

Kaili hiyo aliiongea Diamond akiwa na vijana hao wanaounda kundi hilo Muuh pamoja na Twaa na kuthibitisha ya kuwa kazi hizo ni moja kati ya kazi zake bora na kuwa baada ya mfungo kumalizika atarejea kazini kwa kuachia vibao vikali.

 

Mabantu- Twaa x Muuh

 

Kwa upande wao, Mabantu wamefurahishwa na kitendo hicho cha Simba cha kufanya nao kazi haswa katika kipindi hichi ambacho wameachia EP yao ya University EP ikiwa bado ya moto.

 

Mabantu ni moja kati ya makundi bora zaidi  nchini Tanzania na tayari wameshafanya kazi na wasanii wengine nchini Tanzania kama vile Harmonize, Baddest 47 pamoja na Marioo

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!