Home » Mbunge Osoro: Kuondolewa Kwa Mashtaka Dhidi Ya Wabunge Wa Azimio Hayahusiani Na Mapatano Ya Ruto Na Raila

Mbunge Osoro: Kuondolewa Kwa Mashtaka Dhidi Ya Wabunge Wa Azimio Hayahusiani Na Mapatano Ya Ruto Na Raila

South Mugirango Sylvanus Osoro during a press conference in parliament on 8th.January.2020/EZEKIEL AMING'A


Mbunge wa Mugirango Kusini Sylvanus Osoro amepuuzilia mbali madai kwamba kuondolewa kwa kesi jana Jumatatu dhidi ya viongozi wa muungano wa Azimio kunahusishwa na mwafaka wa kisiasa kati ya Rais William Ruto na kinara wa upinzani Raila Odinga.

 

Hii ni baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) Noordin Haji kuondoa mashtaka yote dhidi ya viongozi sita Mbunge wa Ugunja Opiyo Wandayi, ambaye pia ni Kiongozi wa Wachache katika Bunge la Kitaifa, Seneta wa Kilifi na Kiongozi wa Wachache katika Seneti Stewart Madzayo, Mbunge wa Kilifi Kusini Richard Chonga, Mbunge wa Malindi Amina Mnyazi na madiwani George Obure na Esther ambao walikamatwa wakati wa maandamano ya kuipinga serikali.

 

Akiongea kwenye kipindi cha runinga dakika chache zilizopita, Mbunge Osoro amesema kwamba hakuna uhusiano wowote kati ya matukio hayo mawili na kwamba DPP alikuwa anatekeleza wajibu wake kwa njia ambayo ilitukia baada ya mapatano.

 

Kinara wa walio wengi katika Bunge la Kitaifa ameendelea kuongeza kuwa taasisi huru hazipaswi kuhusishwa na masuala yoyote ya kisiasa, na kuthibitisha kuwa serikali ina nia ya kuheshimu ahadi yake ya kutotumia taasisi hizo kushawishi maazimio ya kisiasa.

 

Akirejelea maoni ya Mbunge Osoro, Mbunge wa Ugunja Opiyo Wandayi amesema bado haijafahamika jinsi DPP aliidhinisha mashtaka hayo kwanza, akibainisha kuwa bado hana uhakika iwapo kujiondoa kulitokana na mapatano hayo.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!