Home » Sifuna Asema Azimio Haitatoa Notisi Za Maandamano Kwa Polisi Tena

Sifuna Asema Azimio Haitatoa Notisi Za Maandamano Kwa Polisi Tena

Chama cha muungano cha Azimio La Umoja One-Kenya hakitatoa tena notisi kwa polisi za maandamano yao ya kila wiki ya kupinga serikali ndio kuali ya Katibu Mkuu wa Chama cha ODM Edwin Sifuna.

 

Chama cha upinzani kimekuwa kikifanya maandamano siku za Jumatatu na Alhamisi kupinga kile kinachodai utawala wa Rais William Ruto kushindwa kupunguza gharama ya maisha na upendeleo katika uteuzi wa Serikali, miongoni mwa masuala mengine.

 

Ingawa Inspekta Jenerali wa Polisi Japhet Koome awali aliambia mrengo unaoongozwa na Raila Odinga kutoa notisi kabla ya maandmano yaliyopangwa, muungano huo umesema hautatoa notisi tena kwa sababu ni haki yao.

 

Sifuna amedai polisi wamekuwa wakivuruga maandamano hayo kwa vurugu badala ya kutoa ulinzi kwa waandamanaji.

 

 

“Hatutatoa tena notisi. Hebu tutekeleze haki zetu chini ya Kifungu cha 37. Maandamano yatatokea yenyewe mahali popote, wakati wowote bila taarifa ya polisi kwa sababu tumegundua taarifa hizo ni mialiko ya wao kututumia vurugu,” aliambia Citizen TV.

 

“Kila kituo kimoja cha polisi jijini Nairobi kimepewa taarifa ya maandamano… dhumuni lake ni kuwaalika kutoa usalama na kuwalinda waandamanaji. Lakini tumegundua kuwa haijalishi ni kwa kiasi gani tunafuata sheria, bado wataendelea kutangaza maandamano yetu kinyume na katiba kuwa ni kinyume cha sheria.”

 

Sifuna aliteta kuwa ghasia na uharibifu wa mali ambao umeshuhudiwa katika Maandmano awamu ya pili iliopita imechochewa na polisi, akiongeza kuwa vikosi vyenye nidhamu vinafaa kuondolewa barabarani ili waandamanaji kuwa watulivu.

 

 

“Lakini kwa hatua ya polisi, maandamano haya yatakuwa ya amani. Ondoa hatua za polisi kutoka kwa mambo haya na uone watu wetu…,” alisema seneta wa Nairobi.

 

Maoni yake yalikuja saa chache baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani Kithure Kindiki kuonya kwamba maandamano ya ghasia hayatakubaliwa popote nchini Kenya.

 

“Pamoja na au bila notisi, maandamano ya aina yoyote ambayo yanajeruhi watu, maafisa wa usalama, biashara na mali yatazuiwa kwa gharama yoyote,” Prof. Kindiki alisema katika taarifa yake kwa vyumba vya habari siku ya Jumatano.

 

Licha ya polisi kuyataja maandamano hayo kuwa kinyume cha sheria, Odinga ameshikilia kuwa ataongoza wafuasi wake kuingia barabarani kutekeleza haki zao za kikatiba.

 

Na wakati watu kadhaa wameuawa, wengine wengi kujeruhiwa na mali kuharibiwa katika maandamano ya awali, kiongozi wa upinzani anashikilia kuwa wamekuwa na wataendelea kuwa wa amani na kuwashutumu polisi kwa kuzua vurugu.

 

Wakati uo huo Rais Ruto anasema hatakuwa na mazungumzo na kiongozi wa upinzani nje ya mipaka ya katiba, kama vile mapatano kati ya Odinga na rais mstaafu Uhuru Kenyatta mnamo Machi 2018.

 

Anasema amekagua matakwa ya Odinga lakini akapata kuwa si ya msingi.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!