Home » AU Yatao Taarifa Kufuatia Tumbo Joto La Kisiasa Nchini Kenya

AU Yatao Taarifa Kufuatia Tumbo Joto La Kisiasa Nchini Kenya

Mkuu wa Tume ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat/picha kwa hisani/

Mkuu wa Tume ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat, amesema ana wasiwasi mkubwa baada ya maandamano ya kuipinga serikali nchini Kenya kugeuka kuwa machafuko huku akitoa wito wa utulivu.

 

Kupitia taarifa yake, mwenyekiti huyo wa Tume ya Umoja wa Afrika amewataka wadau wote nchini  kuwa na utulivu na kuingia kwenye mazungumzo kushughulikia tafauti zao kwa maslahi ya mshikamano na maridhiano ya kitaifa.

 

Mahamat amesema inaonyesha wasiwasi mkubwa juu ya vurugu ambayo imesababisha watu kupoteza maisha, uharibifu wa mali na kukatizwa kwa shughuli za kiuchumi nchini.

 

Amesisitiza kuna haja ya kuwepo kwa mshikamano na uungwaji mkono kwa serikali na wakenya katika juhudi za kuleta umoja wa kitaifa, amani na utulivu nchini

 

Jana, polisi walifyatua vitoza machozi jijini Nairobi na mji wa Kisumu ambako ni ngome ya kiongozi wa upinzani, Raila Odinga, kuwatawanya waandamanaji.

 

Watu kadhaa waliuwawa na mali kuharibiwa. Miongoni mwa mali zilizoharibiwa ni shamba la rais wa zamani, Uhuru Kenyatta, na kampuni ya Odinga.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!