Home » ‘Nilipoteza Zaidi Ya Ksh.3.9M’ Mfanyabiashara Wa Kibra Asema

‘Nilipoteza Zaidi Ya Ksh.3.9M’ Mfanyabiashara Wa Kibra Asema

Hali ya wasiwasi imesalia kuwa juu huko Kibra leo asubuhi ya Jumanne, wakaazi walipoamka ili kutathmini matokeo ya maandamano ya kupinga serikali ya jana Jumatatu.

 

Mamia ya watu wameonekana wakipekua vifusi katika jaribio la kuokoa kile moto mbaya uliozuka Jumatatu jioni ulikuwa umeacha.

 

Miongoni mwa wanaohesabu hasara kubwa ni mfanyabiashara wa eneo hilo aliyetambulika kwa jina moja la John ambaye biashara yake; vifaa na baa viliharibiwa vyote.

 

Kulingana na mfanyabiashara huyo, klabu hiyo, ambako alitafuta riziki ilikuwa na thamani ya karibu Ksh milioni .4 kufikia jana Jumatatu.

 

Leo hii Jumanne, yote yaliyobaki yalikuwa ni majivu, mabati na mawe huku wasiwasi wake ukiwa jinsi atakavyoitunza familia yake.

 

“Hapa ndio tunasomesha watoto, kila kitu ni hapa, sasa vile hii imechomeka, sijui nianzie wapi, hata chakula cha kupelekea watoto hakuna,”

 

Katika kanisa la P.C.E.A, uharibifu unaonekana vipande vya vioo vimetapakaa kwenye sakafu ya kanisa, viti vilivyochomwa wakati wa shambulio hilo.

 

Kulingana na Kasisi Sarah Muriithi, kasisi wa parokia ya P.C.E.A huko Kibera, kanisa hilo lilichomwa moto na wahuni jana Jumatatu.

 

 

Taasisi ya kujifunza iliyounganishwa na kanisa la P.C.E.A pia ilichomwa na kuharibiwa.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!