Home » Karen Nyamu Aandika Jina la Samidoh Shavuni

Seneta mteule Karen Nyamu na mwimbaji wa Mugithi Samidoh Muchoki walionekana wakiwa na wakati mzuri pamoja Jumapili.

 

Karen Nyamu na Samidoh walikuwa wamealikwa nyumbani kwa Waziri wa biashara Moses Kuria ambapo Samidoh aliwatuimbiza wageni.

 

Katika video iliyoshirikishwa rafiki wa Karen, Bakhita Esther, Karen Nyamu alionekana akiwa na wakati mzuri akicheza na babake mtoto.

 

Katika video nyingine, Karen alinaswa karibu na Samidoh na alikuwa ameandika jina lake ‘Samidoh’ kwenye shavu lake.

 

Video hiyo imewaacha Wakenya wakidhani kwamba wawili hao wamerudiana baada ya drama ya uhusiano wao ambayo imeshuhudiwa mtandaoni katika miezi michache iliyopita.

 

Mnamo Februari, wawili hao walionekana wakiwa pamoja na baada ya picha hizo kusambazwa sana kwenye mitandao ya kijamii, mke wa Samidoh Edday Nderitu alimwandikia mumewe ujumbe mrefu kwenye mtandao wa kijamii.

 

Mama huyo wa watoto watatu alisema wamekuwa pamoja kwa miaka 15 lakini miaka michache iliyopita wamejawa na uchungu na fedheha Aliongeza kuwa hatalea watoto wake katika ndoa ya wake wengi na kwa sasa mkewa samidho Edday ametangaza kwamba yuko SINGLE.

 

“Nimekuambia kitu kimoja na ninasema hapa tena sitalea watoto wangu katika familia ya wake wengi, haswa na mwanamke ambaye ananizidi umri kwa zaidi ya miaka 10, hana maadili na heshima kabisa kwa familia yangu.”

 

Desemba mwaka jana, wanawake hao wawili walizozana huko Dubai ambako mwimbaji huyo wa Mugithi alikuwa akitumbuiza na mara baada ya Karen Nyamu kusema kuwa amefanya uamuzi wa kusitisha uhusiano wake na baba wa watoto wake.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!