Home » Rais Ruto Ahimiza Makampuni Ya Ujerumani Kuwekeza Nchini Kenya

Rais Ruto Ahimiza Makampuni Ya Ujerumani Kuwekeza Nchini Kenya

Rais William Ruto amewaalika wafanyabiashara wa Ujerumani kuwekeza katika biashara ndogo ndogo, na za kati nchini Kenya.

 

Rais Ruto amesema Kenya itanufaika na mashirika ya Ujerumani yenye uzoefu zaidi, yaliyopangwa na yenye rasilimali.

 

Ruto amebainisha kuwa sekta hiyo ndiyo uti wa mgongo wa uchumi wa Ujerumani, ikizalisha zaidi ya asilimia 60 ya nafasi za ajira.

 

Rais amekuwa akizungumza leo hii Jumatatu huko Potsdamer Platz mjini Berlin alipokutana na Dkt Markus Jerger, Mwenyekiti wa Der Mittelstand-Ujerumani Chama cha Biashara Ndogo na za Kati (BVMW).

 

Kulingana na Dkt Jerger,sekta hiyo inawakilisha maslahi ya zaidi ya makampuni milioni 3.3 ya watu binafsi nchini.

 

Rais amedai kuwa Serikali imejitolea chini ya Ajenda yake ya Mabadiliko ya Kiuchumi ya kusaidia kuimarisha biashara ndogo ndogo.

 

Baadaye, Rais alifanya mazungumzo na Shirikisho la Muungano wa Maendeleo ya Kiuchumi na Biashara ya Kigeni (BWA) likiongozwa na Mwenyekiti wake Michael Schumann na kukubaliana kuhusu mbinu za kuleta biashara nyingi zaidi za Ujerumani na kimataifa nchini Kenya.

 

Chama hicho tayari kimetaja, uchumi wa kidijitali, miongoni mwa mengine, kama baadhi ya masuala muhimu yanayoweza kuwekezwa.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!