Home » Reuben Kigame Ashtumu Serikali Kwa Kushindwa Kushughulikia Gharama Ya Maisha.

Reuben Kigame Ashtumu Serikali Kwa Kushindwa Kushughulikia Gharama Ya Maisha.

Aliyekuwa mgombea urais Reuben Kigame ameikosoa serikali kwa kile anachodai kushindwa kutatua changamoto zinazowakabili wakenya.

 

Kulingana na Kigame, wabunge wamefumbia macho maswala muhimu yanayowakabili Wakenya na kuelekeza mwelekeo wao kwenye masuala ya siasa.

 

Katika taarifa yake kwa vyumba vya habari, Kigame ametaja matukio kadhaa yaliyotokea katika wiki iliyopita ambapo serikali imefanya maamuzi yasiyofaa ambapo yanaendelea kuzorotesha mapambano dhidi ya gharama ya juu ya maisha.

 

Ametoa mfano wa kuapishwa kwa Makatibu Tawala Wakuu (CAS) siku ya Alhamisi, ambapo alitoa maoni kuwa hatua hiyo ni mzigo usio wa lazima kwa walipakodi na bajeti inayotengwa kwa ajili ya ofisi zao inaweza kugharamiwa kwa miradi mikuu ya maendeleo.

 

Kwenye mpango wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HELB), Kigame alidai kuwa takriban wanafunzi elfu mia140,000 wameachwa bila pesa kwa sababu ya ukosefu wa pesa za masomo, akiitaka Hazina kutoa Ksh. bilioni 5.7 kusaidia kupunguza suala hilo.

 

Wakati uo huo, Rais William Ruto amepuuzilia mbali ripoti kwamba HELB haina pesa taslimu, akidai kuwa serikali imetoa pesa za kutosha kwa HELB kwa ajili ya kuwakopesha wanafunzi kote nchini katika muda wa wiki mbili zilizopita.

 

Itakumbukwa kufikia sasa makatibu wakuu walioteuliwa pia wamezuiwa kushika madaraka na Mahakama Kuu baada ya ombi la kupinga mchakato wao wa uteuzi kuwasilishwa na Chama cha Wanasheria wa Kenya na Taasisi ya Katiba.

 

Mahakama pia ilizuia makatibu hao kupata mshahara, malipo, na manufaa yoyote kusubiri kukamilika kwa kesi.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!