Joh Makini Asimulia Kisa Cha Kuanguka Jukwaani
Rapa wa Tanzania, Joh Makini amefunguka kuhusu tukio la kutisha alilopitia wakati wa tamasha moja alipokuwa jukwaani. Rapa huyo alifichua katika mahojiano na Fredrick Bundala wa SNS kwamba alipata uzoefu wa karibu na kifo baada ya kuanguka jukwaani.
SOMA PIA: Joh Makini Afunguka Juu ya Producer Wa Success
Joh Makini alielezea tukio hilo la katisha, ambalo lilitokea miaka kadhaa iliyopita wakati wa tamasha la Castle Lite Unlock Festival alipokuwa akitumbuiza wimbo wake maarufu “Don’t Bother” aliomshirikisha AKA kutokea Afrika ya kusini mwaka 2019 katika uwanja wa Posta. Kulingana na rapper huyo, alikuwa katikati ya maonyesho yake wakati ghafla alipoteza usawa na kuanguka kwa nguvu kwenye jukwaa.
Katika mahojiano hayo, Joh Makini alisema “Niliwahi kuanguka kwenye Stage, huwezi kuamini….unajua nilianguka kwenye stage alafu nilianguka katika mazingira ambayo ningeweza kufa pale”
Ikumbukwe kuwa hivi karibuni Joh Makini aliachia EP yake ya Wave ikiwa ni EP yake ya kwanza yenye jumla ya nyimbo sita.