Home » “Mke Wangu Ana Miaka 21,” Mzee Wa Miaka 60 Aeleza

Mwanaume mmoja wa Nigeria hatimaye amezungumza baada ya kutuhumiwa kuoa mtoto mdogo.

 

Mwanamume mwenye umri wa miaka 60 Aminu Danmaliki alikabiliwa na kashfa kutoka kwa umma ambao walimshutumu kwa kuoa msichana wa miaka 11 kutoka jimbo la Kano Nigeria baada ya picha za harusi yao kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.

 

Danmaliki katika chapisho kwenye ukurasa wake wa Facebook Jumatano alisema mkewe ana umri wa miaka 21, wanapendana na hakulazimishwa kumuoa.

 

“Ndoa yangu ya hivi majuzi na Sakina imezua mvutano mkubwa na madai yasiyo na msingi kuwa nilioa msichana mdogo, wengine walidai ana miaka 11 na alilazimishwa kunioa, huo sio ukweli, video ya harusi ilisambaa, tukaamua kunyamaza lakini walishauriwa kueleza mambo ya kweli.Hapa ni: Mke wangu mpendwa ana umri wa miaka 21. Alinichagua mwenyewe kuwa mume wake, nami nilimpenda pia.”

 

Danmaliki alisema matakwa yake ni kwamba watu wanaochukia na wanaotembelea mitandao ya kijamii waone ukweli kwenye picha aliyoiweka kwenye mitandao ya kijamii, na kumruhusu yeye na Sakina kufurahia fungate yao.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!