Home » Uchunguzi Wa Maiti Wafichua Kilichomuua Mchungaji Elizabeth

Ripoti ya uchunguzi wa maiti imefichua kilichomuua Mchungaji Elizabeth nyumbani kwa Mwanamuziki wa Injili wa Kikuyu Dishon Mirugi.

 

Zoezi la uchunguzi wa maiti iliyofanywa katika chumba wafu cha Kenyatta ambapo umefichua kuwa Wanjiru alifariki kutokana na shinikizo kwenye shingo, ingawa haikujulikana ikiwa ni kunyongwa au kujinyonga.

 

Wataalamu wa magonjwa wamechukua sampuli zaidi kwa uchambuzi zaidi.

 

Aidha Familia imekanusha madai kwamba Mchungaji Elizabeth alijitoa uhai.

 

Familia hiyo inadai kuwa alilalamika kupokea vitisho kutoka kwa mtu wa Mungu ambaye alikuwa amemkopesha Ksh.700,000 ili kuanzisha kanisa lake kwa ahadi ya kumlipa.

 

Marehemu Kasisi Elizabeth Wanjiru alitoweka siku ya Ijumaa baada ya kufahamisha dadake kwamba alikuwa akienda kwa Mirugi kuomba pesa zake pesa taslimu, ndipo wakapokea ripoti kutoka kwa polisi kwamba alipatikana akiwa amefariki.

 

“Alinipigia simu masaa ya saa saba akaniambia dadangu ile siku nimeishi kukuambia imefika kwa sababu sasa nimeamua kwenda kwa Dishon kuitisha ile pesa yangu. Saturday tulishinda tukimpigia simu hakushika wala hakurudisha messages…Sunday tukamjaribu asubuhi tukamkosa, nilijaribu kupiga hiyo simu tena ikashikwa na DCI akaniambia dada yenu hayuko tena,” alisema Dada yake Esther.

 

Dishon Mirugi alisema kuwa alimwacha Elizabeth nyumbani kwake akifanya usafi na aliporudi nyumbani, alimkuta akiwa amening’inia kwenye kabati lake la nguo.

 

Dishon anasemekana kuzunguka na mwili wa marehemu kasisi kwa saa kadhaa kabla ya kuupeleka katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya KU baadaye jioni.

 

Mirugi ambaye alikamatwa siku ya Jumapili alifikishwa katika Mahakama ya Makadara na polisi wakitaka kumshikilia kwa siku 14.
Mwanamuziki huyo atasalia rumande hadi Machi 24 mahakama itakapotoa uamuzi iwapo itamwachilia kwa dhamana au la.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!