Home » Mkewe Atsu Na Watoto Wameondoka Ghana Siku 3 Baada Mazishi Ya Mumewe

Mkewe Atsu Na Watoto Wameondoka Ghana Siku 3 Baada Mazishi Ya Mumewe

Claire, mke wa marehemu nyota  wa black stars ya Christian Atsu ameondoka nchini Ghana siku tatu tu baada ya kumaliza shughuli ya kumzika aliyekuwa mumewe.

 

katika kurasa yake wake Instagram, Claire amabye ni raia wa ureno, alituma picha za majonzi akimpa buriani za mwisho Atsu na kuwaandikia wananchi wa Ghana ujumbe wa kwaheri, akisema kwamba Mungu akipenda wataonana tena siku moja.

“Asante Ghana, hadi tutakapokutana tena, Christian Tunakupenda,” kasema claire.

Claire, familia yake na watoto walikuwa nchini Ghana siku ya Ijumaa tarehe 17 Machi kwa maziko ya Wing’a  huyo wa Ghana.

Inasemekana Claire  na watoto walitembelea kaburi lake mara ya mwisho kabla ya kurejea Ulaya. Atsu, mwanasoka mwenye kipawa cha hali ya juu, alipoteza maisha wakati wa tetemeko la ardhi lililoikumba Uturuki.

 

Tetemeko la ardhi lilisababisha vifo vingi Uturuji.

Atsu  alizikwa nyumbani kwao jiji Ada nchini Ghana mnamo Machi 17, 2023.

Ziara ya kihisia ya familia kwenye kaburi la Atsu ilikuwa fursa kwao kutoa heshima zao za mwisho kwa mume na baba yao wapendwa.

 

Mke na watoto wake walikuwa wamefadhaika sana, na uchungu wa kufiwa ulionekana wazi katika machozi yao na maneno yao ya huzuni. Ziara hiyo ilikuwa fupi, lakini iliwaruhusu kupata muda wa kuwaaga kabla ya kurudi Ureno.

 

Atsu alikuwa mwanasoka mashuhuri ambaye alichezea vilabu mbali mbali, vikiwemo Chelsea, Everton, na Newcastle United. Pia alikuwa mchezaji muhimu wa timu ya taifa ya Ghana, ambapo alijulikana kwa kasi yake, wepesi, na ustadi uwanjani.

 

Baadhi ya wanamitandao walihisi kwamba mwanamke huyo anakwenda kinyume na mila na tamaduni za Kiafrika kwani mjane hafai kuondoka katika boma lake baada ya maziko, hadi angalau kwa siku 40.

 

 

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!