Home » Nyota Wa Zamani Wa Arsenal Na Manchester City Astaafu

Nyota Wa Zamani Wa Arsenal Na Manchester City Astaafu

Picha kwa hisani ya GETTY IMAGES

Mshambulizi wa zamani wa Arsenal,Tottenham, crystal Palce  na Manchester City inayoshiriki ligi kuu uingereza Emmanuel Adebayor ametangaza kustaafu kucheza soka akiwa na umri wa miaka 39.

 

Adebayor amekuwa katika taaluma ya soka kwa zaidi ya ya miaka 22. Amecheza katiki ligi kadhaa duniani ikiwemo  Ufaransa, Uingereza, Uhispania, Uturuki, Paraguay na nchi yake ya Togo. Alifunga mabao 97 katika mechi 241 kwenye Premier League, akichezea Arsenal, Manchester City, Tottenham na Crystal Palace.

 

 

Rekodi hiyo inamweka katika nafasi ya 35 kwenye orodha ya wafungaji mabao mengi katika Ligi ya Uingereza.

 

 

Adebayor pia ameitumikia vya Metz na Monaco ya Ufaransa, Real Madrid ya Uhispania na Istanbul Basaksehir ya Uturuki.

 

 

“Kutoka Baharini, juu hadi chini, kazi yangu kama Mchezaji imekuwa safari ya kufana sana. Asante kwa mashabiki wangu kwa kuwa nami popote niendapo. Nashukuru sana kwa kila kitu. Nina furaha nyingi kwa kile kitakachokuja!” aliandika kwenye Instagram.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!