Home » Watu 87 Wakamatwa Katika Maandamano Afrika Kusini

Looters outside a shopping centre alongside a burning barricade in Durban, South Africa, Monday July 12, 2021. Police say six people are dead and more than 200 have been arrested amid escalating violence during rioting that broke out following the imprisonment of South Africa's former President Jacob Zuma. (AP Photo/Andre Swart)

Takriban watu 87 wamekamatwa leo Jumatatu asubuhi wakishiriki maandamano nchini Afrika Kusini.

 

Waandamanaji 87 walikuwa sehemu ya Waafrika Kusini wengi waliotii wito wa maandamano ya nchi nzima uliotolewa na chama cha upinzani cha Economic Freedom Fighters (EFF), kinachoongozwa na Julius Malema.

 

Polisi wa Afrika Kusini wanasema kuwa watu hao walikamatwa katika maeneo tofauti nchini humo.

 

Maelfu ya Waafrika Kusini waliingia mitaani leo hii Jumatatu, katika maandamano yaliyopewa jina la ‘National Shutdown’ huku nchi hiyo ikikabiliana na masuala mengi, miongoni mwao; ukosefu wa ajira, kukatwa kwa umeme na ufisadi wa ovyo.

 

Video kadhaa zilizowekwa kwenye Twitter mapema leo zimeonyesha waandamanaji wakimiminika mitaani kwa idadi kubwa huku kukiwa na madai kwamba wengi walikuwa wameingia mitaani mapema saa moja hivi..

 

Waandamanaji wanamtaka rais wao Cyril Ramaphosa kujiuzulu wakimtuhumu kwa kushindwa kushughulikia masuala hayo.

 

Chama hicho pia kiliwashauri wafanyikazi wasio wa lazima kubaki nyumbani, au wajiunge na maandamano, wakidai kuwa huo utakuwa mwanzo wa mapinduzi yasiyozuilika.

 

Maandamano mengine yanashuhudiwa Kenya ,,Nigeria,,Tunisia Na marekani kupinga sera za serikali

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!