Home » Gor Mahia Na KCB Wacheza Sare Mechi Ya KPL

Gor Mahia Na KCB Wacheza Sare Mechi Ya KPL

Viongozi wa ligi kuu nchini kenya Gor mahia wametoa sare ya nunge dhidi ya KCB katika mechi ya KPL. Mechi hiyo ya kupendeza ilipigwa katika uga wa kimataifa wa Nyayo, Nairobi.

 

 

Pande zote Mbili zilipoteza nafasi za wazi ya kufunga bao lakini Gad Mathews wa Gor Mahia na mwenzake wa KCB Bryne Odhiambo walikuwa ngangari langoni.

 

 

Hata hivyo, sare hiyo bado inaiweka Kogalo juu ya jedwali na alama 42 ikifuatiwa na KCB na alama 37. Omalla benson bado anaongoza kwa ufangaji mabao akiwa na mabao 19 na kufuatiwa na Elvis Rupia na mabao 12.

 

 

Katika mechi zingine zilizo  sakatwa jana, AFC Leopards iliifunga posta Rangers bao moja kwa nunge, Police FC wakatoa sare ya 2-2 na nzoia sugar.

 

 

Bandari waliifunga Mathare United moja kwa yai kisha Sofapaka wakawalaza kakamega homeboyz 3-1.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!