Home » Katibu Mkuu Wa Zamani Wa KANU Nick Salat Ajiunga Na UDA

Katibu Mkuu Wa Zamani Wa KANU Nick Salat Ajiunga Na UDA

Aliyekuwa katibu mkuu wa chama anzilishi cha KANU nick salat amejiunga  rasmi na chama tawala cha UDA  kinachoongozwa na rais William Ruto.

 

 

Salat alitia sahihi na chama hicho  mapema jumatano asubuhi akiwa ameandamana na viongozi wengine kutoka kaunti tofauti tofauti nchini waliyoamua kukigura chama cha baba na mama. Nick amesema hajashurutishwa na mtu yeyote kufanya uomuzi huo

 

 

Salat alipokelewa chamani na katibu mkuu wa UDA cleophas Malala ambaye amesema nia yake ni kuipa UDA sura ya kitaifa.

 

 

 

‘’Tumeamua kusonga mbele. Kwa sasa tuko kwa nyumba nyingine itakayo tusaidia katika azma yetu ya kisiasa siku za usoni’’ kasema salat

 

 

Salat amesema uamuzi wa kukihama KANU ni baada yake kufeli kutimiza ndoto yake kwa wakenya.

 

Mbunge huyo wa zamani wa Bomet Ya kati alitofautiana na KANU na kutimuliwa na kutokuwa na maadili mema chamani.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!