Harmonize Aanzisha Podcast
Mbabe wa ngoma ya I am Single Rajab Ibrahimu ambaye pia anajulikana kama Harmonize amekuja kivingine mara baada ya kuanzisha Podcast yake aliyoipa jina la Never Give Up ambayo inapatikana Boomplay pekee.
Katika podcast hiyo Harmonize ameanza kwa kueleza safari yake ya mapenzi baada ya kuumizwa mara ya kwanza kwa kunyang’anywa Jiko katika hatua za kuoana na mpenzi wake wa kipindi hicho.
SOMA PIA:Ruby Apata Mtoto Wa Pili
Pia panda shuka za mishe za mjini baada ya kutoka Mtwara na kuhamia katika jiji la Pilika pilika Dar es salaam na kuanza maisha yake Tabara Segerea Bonyokwa.
Mwanzo lengo lilikuwa ni kuwa mchezaji bora wa mpira wa miguu huku uimbaji ukiwa kama sehemu ya burudani kwake mpaka pale alipopata nafasi katika muziki na kuitumia nafasi hiyo kwa nguvu zote huku akimtegemea Mungu.