Home » Mohammed Ali Adai Maisha Yake Yamo Hatarini

Mbunge wa Nyali Mohammed Ali anadai kuwa maisha yake yamo hatarini.

 

Mohammed Ali amechapisha picha za risasi zilizopitia dirishani kwake zikimlenga akisema kuwa watu wanaofanya jaribio la kumuua hawatafaulu huku akifichua kuwa hilo limetokea karibu mara tano na kuongeza kuwa hakuna binadamu anayeweza kumuua mtu mwingine isipokuwa tu mapenzi ya Mungu.

 

Mwanahabari huyo aliyegeuka kuwa mwanasiasa alibainisha kuwa washambuliaji walikuwa wakitamani kumwona amekufa ila hawataweza.

 

Kisa hicho kimepokea maoni tofauti kutoka kwa wafuasi wake,

 

@Judy Wawira-Kwa hiyo unataka tuamini watu wanafuata maisha yako kama mwanasiasa lakini sio wakati unafanya jicho pevu sindio? Watu si wajinga bana

 

@Wanagai-nafasi ya risasi hii na aina ya bunduki iliyotumika vinahitaji kutambuliwa ili kubaini umbali kamili ambao bunduki ilifyatuliwa. Huyu ni mpiga risasi anayejificha mahali fulani kwenye jengo hilo au mahali pengine kando yake.

 

@Fahiryabas-Je nyie mnaweza kumpa amani kijana huyu ili aweze kuwatumikia wananchi waliomchagua

 

@muleigibson- Sasa unatengeneza showbiz nyingine, ili tupitishe roller coaster nyingine…ili tusiwahi kujadili gharama za juu za maisha.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!