Home » Eric Omondi Aadhimisha Miaka 41 Ya Mazazi

Mwigizaji maarufu Eric Omondi ametuma ujumbe wa matumaini kuadhimisha miaka 41 ya kuzaliwa kwake.

 

“Ninapofikisha miaka 41 leo naweza tu kutafakari Safari na Kujiandaa kwa mustakabali mwema kwa ajili yangu na Wananchi wangu. Kama vile Waisraeli walivyotangatanga Jangwani kwa miaka 40, nahisi huu ndio Mwaka tunaoanza Safari yetu katika AHADI.. Karibuni sana maisha yetu yatatiririka Maziwa na Asali kwa sababu haya ni MAPENZI YA MUNGU,” aliandika.

 

Siku yake ya kuzaliwa inajiri siku chache baada ya Omondi kukamatwa kwa maandamano kinyume cha sheria nje ya majengo ya bunge kuhusu kile alichokitaja gharama ya juu ya maisha.
Mcheshi huyo alikamatwa mnamo Februari 21 pamoja na wengine 16 kando ya Barabara ya Bunge na kufikishwa mahakamani Februari 22 ambapo alishtakiwa kwa kuandaa maandamano kinyume cha sheria na kuachiliwa kwa dhamana ya pesa taslimu Ksh10,000.

 

Mnamo Jumatatu, Machi 6, alinyimwa maagizo ya kutarajia baada ya mahakama kukataa kutoa amri ya kuwazuia polisi kumkamata na kumtisha, kwa kuwa kesi bado iko mahakamani.
Katika chapisho la mtandao wa kijamii, Omondi alifananisha umri wake mpya na Waisraeli akisema unaashiria mwanzo wa maisha mapya Katika uamuzi wake, Hakimu Mkuu wa Milimani Lucas Onyina alisema kuwa haiko ndani ya mamlaka ya mahakama yake kutoa maagizo ya kutarajia, kwa kuwa amri hizo zimetengwa kwa mahakama za mamlaka ya juu.

 

Wakili Danstan Omari aliiambia mahakama kuwa mteja wao alikamatwa Machi 1, alipokuwa akisambaza chakula kwa wanyonge, katika zoezi la ugawaji wa chakula, kwa sababu alikiuka masharti ya dhamana yaliyotolewa na mahakama hiyo hiyo.

 

Aidha alifahamisha mahakama kuwa Omondi baada ya kukamatwa alihamishwa kutoka kituo kimoja cha polisi hadi kingine bila kufunguliwa mashtaka wala kufikishwa mahakamani.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!