Home » Sheeba Karungi Apinga Bifu Baina Yake na Spice Diana

Staa wa muziki kutoka nchini Uganda Sheebah Karungi kwa mara ya kwanza amenyoosha maelezo kuhusu bifu yake na msanii mwenzake Spice Diana.

 

Kwenye mahojiano yake hivi karibuni, mrembo huyo amethibitisha kuwa hajawahi kuwa urafiki na Spice Diana huku akisema kwamba kufanya kwao kazi ya pamoja ilitokana na shinikizo walizokuwa wakipata kutoka kwa mashabiki.

 

Sheebah amemshauri Spice Diana kuwapuuza watesi wake na kuangazia zaidi muziki wake kwa kuwa ni moja kati ya wadada ambao wana vipaji sana kwenye muziki.

 

Hata hivyom amefichua kuwa hajali kabisa kuhusu kitendo cha hitmaker huyo wa “Siri Regular” kufuta urafiki wao kwenye mitandao ya kijamii.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!