Home » Kindiki Aibuka Bora Katika Utendakazi

Waziri wa Madini na Masuala ya Bahari Salim Mvurya na mwenzake wa Kazi na Ulinzi wa Jamii Florence Bore wameorodheshwa miongoni mwa Mawaziri waliotekeleza majukumu yao kwa kiwango cha chini mno kwa Wakenya, kulingana na ripoti mpya ya kampuni ya utafiti ya Infotrak.

 

Kura ya maoni ya Sauti ya Wananchi iliyotolewa leo Jumanne inaonyesha kwamba Gavana huyo wa zamani wa Kwale, ambaye alichukua wadhifa wa Monica Juma Oktoba mwaka jana, ana umaarufu wa asilimia 0.2, pamoja na Bore aliyechukua wadhifa huo kutoka kwa Simon Chelugui.

 

Wengine waliopata alama ndogo ya asilimia 1 ni Davis Chirchir wa Nishati na Petroli asilimia 0.5 simony Chelugui wa Ushirika na Biashara Ndogo, Ndogo asilimia 0.7 Njuguna wa fedha Ndung’u Hazina asilimia 0.4 Roselinda Soipan Tuiya wa Mazingira asilimia 0.4 na Rebecca Miano wa Maendeleo ya Kikanda asilimia 0.3).

 

Kwa upande mwingine, Waziri wa Mambo ya Ndani Kithure Kindiki ameongoza orodha hiyo kwa kupata asilimia 27, akifuatiwa na mwenzake wa Elimu Ezekiel Machogu asilimia 12% na Ababu Namwamba wamichezo kwa asilimia 8.

 

Ripoti hiyo imetoa alama za kiraia juu ya utendakazi wa wizara katika siku 100 za kwanza chini ya makatibu wapya wa baraza la mawaziri.
Kwa mujibu wa wizara, wakenya wameorodhesha wizara ya mawasiliano na habari kama wizara iliyofanya vizuri zaidi kwa ikipewa asilimia 54, ikifuatiwa na wizara ya Barabara na Uchukuzi asilimia 50 na Ulinzi asilimia 49.

Wizara ya fedha pamoja na Nishati zimeorodheshwa chini zaidi kwa asilimia 35, ikifuatiwa na Maji, Usafi wa Mazingira na Umwagiliaji asilimia 40.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!