Home » Tanzania Kuboresha Mazingira Ya Uwekezaji
Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Philip Mpango, amewakaribisha wawekezaji kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya (EU) kuja kuwekeza nchini kwenye maeneo yanayoendana na mahitaji, ili kuiwezesha nchi hiyo kutimiza malengo ya Dira ya Taifa  ya 2025 na kuikuza kutoka uchumi wa kati wa chini hadi uchumi wa kati wa katikati.
Hii ni kutokana na Tanzania kuwa na  fursa nyingi za uwekezaji  ikiwemo kilimo, viwanda vya kuongezea thamani mazao ya kilimo,  viwanda vya dawa na vifaa tiba, ujenzi, sayansi, teknolojia, maendeleo ya viwanda katika kizazi cha nne (4th Industrial Evolution).
Wito huo ameutoa wakati wa ufunguzi wa Kongamano la aina yake la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Nchi za Umoja wa Ulaya linalofanyika leo tarehe 23 na kutarajiwa kumalizika kesho 24 Februari, 2023  jijini Dar es Salaam.
Kongamano hilo lililojumuisha zaidi ya washiriki 800 kutoka nchi za Umoja wa Ulaya na Tanzania lililolenga kuwaunganisha washiriki hao katika kongamano hilo na kuonyesha fursa za uwekezaji zilizopo Tanzania.
“Kwa upande wa kilimo, tumeongeza bajeti ya kilimo kwa zaidi ya asilimia 800 kwa mwaka huu wa fedha tunaotekeleza, hii inaonyesha utayari wa serikali yetu katika kuwekeza kwenye kilimo, kutokana na janga la UVIKO-19 pamoja na vita inayoendelea Urus na Ukrein imetuletea changamoto ya chakula Duniani, hivyo tuko tayari kushirikiana na wezentu kuwekeza ili tuweze kulima chakula ndani ya Taifa letu kwani zaidi ya asilimia 60 ya ardhi yetu ipo tayari kwa kilimo na haijalimwa” 
“Kuhusu viwanda vya dawa na vifaa tiba, UVIKO-19 na vita kati ya urusi na Ukrein imetuletea athari kwenye eneo hilo katika kupata dawa na vifaa tiba,  hivyo tunawakaribisha mje kuwekeza ili tupate ujuzi na kutengeneza ajira kwa vijana wetu” Amesema Dkt. Mpango
Mbali na hayo Dkt. Mpango amesema Serikali imedhamiria  kuboresha mazingira ya uwekezaji na ufanyaji biashara kwa kuendelea kurekebisha sheria mbalimbali na kuboresha mifumo ya  ulipaji kodi ikiwemo sera za ulipaji kodi kwa nchi kumi
Dkt. Mpamgo ameongeza kuwa “Serikali itaendelea kuimarisha kituo cha uwekezaji Tanzania ( TIC) na Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA), Kuimarisha upatikanaji wa umeme, Uendelezaji wa Bandari ya Dar es salaam, Tanga  na Mtwara, Bandari kavu ya kwala , ujenzi wa barabara na reli, na uanzishaji wa Sheria ya Uwekezaji ya 2022 ikifuta ile ya 1997 “
Kwa upande wake Waziri wa uwekezaji, Viwanda na Biashara wa nchi hiyo Dkt. Ashatu Kijaji amesema wanatamani kuona mazingira yaliyo bora, wawekezaji wanapoingia ndani ya Taifa wapokelewe na muda wa kupata vibali vyote upungue kutoka siku 30 mpaka siku saba.
Amesema katika Sheria ya uwekezaji ya mwaka 2022 wameongeza kipengele ambacho mikataba yote ya vivutio itakayosainiwa utekelezaji wake utaanza kwa haraka.
Kwa upande wake waziri wa Mambo ya Nje, Biashara na vivutio vya uchumi  wa Ufaransa Olivier Becht,   amesema lengo la Ufaransa ni kuimarisha uwekezaji  Tanzania na Afrika Mashariki kwani Serikali yake imekuwa ikishirikiana na Serikali ya Tanzania hususani katika sekta za kimkakati.
Naye Makamu wa Rais wa  benki ya Uwekezaji ya Umoja wa Ulaya (EIB),  Thomas Östros, amesema  Benki hiyo ya EIB imerudi nchini baada ya UVIKO- 19 na iko tayari kufanya uwekezaji mkubwa  wenye thamani ya EUR milioni 540 kwa kuwawezesha wawekezaji na wafanyabiashara nchini wakiwemo wananwake , maji, utalii na na kampuni zinazojihusisha  wna uchumi wa Blue.
” Hii itafanyika kupitia ushirikiano na kifedha kati ya EIB na CRDB, NMB, na KCB  pamoja na makubaliano yaliyofanyika leo kati ya  makampuni ya Umoja wa Ulaya na Tanzania  makampuni ya Tanzania itakayowawezesha kuwekeza na kupanua biashara zao  hususani katika utalii, uvuvi.”
Aidha, katika kongamano hilo, hati za makubaliano tatu zimetiwa saini ambapo hati ya makubaliano ya  huduma ya usafiri wa anga uliotiwa saini na waziri wa ujenzi na uchukuzi Profesa Makame Mbarawa na Waziri wa mambo ya nje, biashara na vivutio vya uchumi wa Ufaransa Olivier Becht ambapo makubaliano hayo yatawezesha  kuongeza idadi ya safari za ndege kati ya tanzania na ufaransa ikiwemo safari za moja kwa moja kutoka Dar e salaam kwenda ufarasa  ifikapo mwezi june 2023 kisiwa cha mayotte ambapo makampuni ya ndege ya tanzania yataruhusiwa kusafiri moja kwa moja hadi kisiwa hichokwanza  Tanzania and French direct Zanzibar to France.
Vile vile wametia saini hati ya makubaliano iliyohusu ujenzi wa Mradi wa uzalishaji wa umeme wa Kakono Hydro Power utakaojengwa Mkoani Kagera nchini humo uliofadhiliwa na Benki ya Maendelo Afrika chini ya ufadhili wa Umoja wa Ulaya.
Hati nyingine ya makubaliano iliyotiwa saini ni kati ya bandari ya Antwerp-Bruges International na Mamlaka ya Bandari ya Tanzania ambao utaongeza  usimamizi wa bandari na kuimarisha miundombinu ya bandari ikiwemo bandari kavu na bandari za maziwa na kuiongezea uwezo bandari hiyo  ili kuongeza ufanisi wa bandari ya Tanzania.
Mkurugenzi wa mamlaka ya bandari Tanzania-TPA, Plasduce Mboso Amesema Mkataba kati ya TPA na bandari ya ubelgiji utaongeza ufanisi katika shughuli za bandari na kuzidi kukuza uchumi wa nchi kutokana na mapato yatakayo kusanywa na bandari hiyo.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!