Waziri Wa Mambo Ya Ndani Aamuru Polisi Kuwafuata, Kuwakamata Wahamiaji Haramu
Maafisa wa polisi wako chini ya maagizo ya kuwasaka na kuwakamata watu wote ambao wako nchini kinyume na sheria.
Waziri wa Mambo ya Ndani Prof. Kithure Kindiki ametoa onyo kwamba baadhi ya wahamiaji haramu wanaweza kupanga njama ya kutekeleza uhalifu wa kutisha nchini.
Waziri kindiki amesema changamoto ya wageni haramu, sawa na ile ya pombe haramu na majengo duni inapaswa kuwa mstari wa mbele kwa maafisa wetu wa kitaifa wa kutekeleza sheria wakiongozwa na timu za kijasusi za kaunti na mkoa.
Kulingana na Prof Kindiki, Kenya inakumbwa na tatizo kubwa ambapo watu ambao si raia wa Kenya wamekuwa wakivuka kutoka mataifa mengine na kuendelea kuishi na kufanya kazi kinyume cha sheria. Alisema ujumbe huo kwa baadhi yao kinyume na sheria.
Kindiki ambaye alikuwa Ruiru wakati wa kuanzishwa kwa shule ya msingi ya GSU mnamo Jumatatu alifichua kwamba wengi wao wanakaa katika kaunti jirani za Nairobi na Kiambu.