Home » Magavana Walaumu Serikali Ya Kitaifa Kwa Ucheleweshaji Wa Fedha

Magavana Walaumu Serikali Ya Kitaifa Kwa Ucheleweshaji Wa Fedha

Magavana wa Kaunti wameorodhesha ufadhili usiotosha, kufuata kanuni za ugavi wa mapato na ucheleweshaji wa mara kwa mara wa kuidhinisha matumizi, kuwa changamoto kuu zinazokabili vitengo vilivyogatuliwa tangu kutangazwa kwa sheria ya 2010.

 

Baraza la Magavana katika ripoti yake sasa wameelezea masuala makuu yanayoathiri utendakazi bora katika utekelezaji wa Ugatuzi.

 

Mwenyekiti wa Kamati ya Masuala ya Kisheria ya baraza hilo ambaye pia ni Gavana wa Makueni Mutula Kilonzo Jnr anasema matumizi ya kaunti yanacheleweshwa kila mara na Mdhibiti wa Bajeti Margaret Nyakangó.

 

Kulingana na Mutula, usimamizi wa bajeti unachukua muda mrefu kuidhinisha maombi yao, akiongeza kuwa kisheria, lazima iidhinishe matakwa yote yaliyotolewa na kaunti kabla ya kutumia pesa hizo.

 

Magavana hao wamesema kaunti hizo zinakabiliwa na matatizo ya pesa kutokana na uhaba wa fedha na kucheleweshwa kwa utoaji wa fedha na Hazina ya Kitaifa, hatua waliyosema inapunguza kasi ya huduma na maendeleo.

 

Katika hotuba yake kwa kamati ya wanachama tisa, Mutula aliiomba kamati hiyo inayoongozwa na seneta Mohammed Abass wa (Wajir) kuingilia kati ili kuhakikisha kuongezwa kwa ufadhili wa fedha hizo kwa wakati na Hazina ya Kitaifa.

 

Kwa sasa, kaunti hizo zinadaiwa takriban Shilingi milioni mia moja za Desemba, Januari na Februari, hali ambayo magavana wanasema imeathiri utendakazi kaunti hizo.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!