Home » Matiang’i Yupo Njia Panda

Idadi isiyojulikana ya maafisa wa polisi mashuhuri walionekana nyumbani kwa aliyekuwa Waziri wa Usalama wa Ndani Dkt Fred Matiang’i huko Karen, Nairobi jana Jumatano usiku.

 

Sababu ya operesheni ya usalama katika nyumba ya waziri huyo wa zamani wa usalama haikuweza kufahamika mara moja.

 

Imebainika kuwa waziri huyo wa zamani alikuwepo nyumbani wakati wa kisa hicho akiandamana na mawakili wake wakiongozwa na Danstan Omari ambaye alidai kuwa maafisa hao walinuia kumkamata Matiang’i.

 

Akihutubia wanahabari nje ya nyumba ya Waziri huyo wa zamani, wakili Danstan Omari alisema maisha ya Matiang’i yalikuwa hatarini, akiongeza kuwa hawakufahamu nia gani ya uvamizi uliokusudiwa dhidi ya nyumba hiyo.

 

Aliongeza kuwa mawakili wengi watamlinda Matiang’i usiku kucha ili kuhakikisha maafisa wa usalama wanafuata sheria.

 

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga, ambaye alifika nyumbani kwa waziri huyo wa zamani mwendo wa saa kumi jioni alikashifu vikali oparesheni hiyo ya usalama akiitaja kuwa “haikubaliki kabisa.”

 

Timu ya maafisa wa usalama waliopatikana nyumbani kwa Matiang’i inaripotiwa kutoroka mara baada ya vyombo vya habari kutangaza habari za operesheni hiyo.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!