Washukiwa Wa Mauaji Ya Edwin Chiloba Waachiliwa
Mahakama mjini Eldoret imewaachilia huru washukiwa wanne wanaohusishwa na mauaji ya mwanaharakati wa (LGBTQ) Edwin Kiprotich Kiptoo almaarufu Chiloba.
Wanne hao wameachiliwa baada ya upande wa mashtaka kusema hauna ushahidi wa kutosha kuwashtaki, kufuatia siku 21 za uchunguzi ambao ulikuwa umekubaliwa na mahakama.
Mwana misuli Dennis Litali ameachiliwa huru huku washukiwa wengine watatu wakiripoti kwa polisi kila mwezi kwa miezi mitatu.
Jaji Richard Odenyo hata hivyo ameagiza mshukiwa mkuu Jacktone Odhiambo kujibu mashtaka ya mauaji katika Mahakama ya Juu.
Odhiambo alifikishwa katika Mahakama Kuu mara moja kujibu mashtaka ya mauaji.
Chiloba alipatikana ameuawa na mwili wake kuhifadhiwa kwenye sanduku la chuma ambalo lilitupwa katika kijiji cha Hurlingham karibu na Kipkaren mnamo Januari 3 2023.