Koigi Wa Wamwere Adai Ziara Ya Ruto Nyanza Ni kutulizo Cha Joto La kisiasa
Mchanganuzi wa kisiasa Mwangi njui anasema mapokezi ya hali ya juu ya Rais William Ruto katika ukanda wa Nyanza ni mbinu ya kuleta salamu za polepole kati ya rais na kiongozi wa Azimio Raila Odinga.
Njui amesema Raila ana hulka ya kuungana na viongozi wanaomshinda, na kutabiri kwamba hivi karibuni wakenya watashuhudia wawili hao wakifanya kazi pamoja.
Mbunge wa zamani wa Subukia Koigi wa Wamwere amesisitiza hayo akisema Raila hana lengo lolote la kuongoza ofisi ya upinzani hapa nchini. Koigi hata hivyo anasema kwa wawili hao kufanya kazi pamoja, lazima kuna mkono wa nguvu za nchi za Magharibi.
Njui wakati uo huo amesema naibu wa rais Rigathi Gachagua ndiye anaongoza katika kuwapatanisha Raila na rais Ruto. Njui ametaka serikali kuchambua sakata zote za ufisadi na kuanika wahusika badala ya kuwavumilia.
Hali kadhalika Koigi amezisuta serikali za Jubilee na Kenya Kwanza kwa kushindwa kupigana na ufisadi. Kulingana na Koigi, taifa haliwezi kujikimu iwapo serikali haitapiga vita ufisadi kikamilifu.