Home » Dj Brownskin Kukaa Rumande Wikendi Hii

DJ Brownskin almaarufu Michael Macharia Njiiri anayeshutumiwa kwa kusaidia kujiua kwa mkewe mwaka jana atazuiliwa wikendi hadi ripoti yake ya awali ya dhamana iwasilishwe mahakamani.

 

DJ huyo ambaye alikuwa tayari kuachiliwa kwa dhamana siku ya Alhamisi, alipata pigo baada ya upande wa mashtaka kuambia mahakama kwamba ripoti ya awali ya dhamana haikuwa tayari na kuomba muda zaidi.

 

Alifika mbele ya Hakimu Mkuu wa Milimani, Lukas Onyina ambaye aliagiza kesi hiyo kuwasilishwa Juni 19 ripoti hiyo itakapokuwa tayari.
Kesi hiyo itatajwa Juni 19.

 

Mnamo Jumatano, mahakama iyo hiyo ilikataa kuruhusu ombi la DJ Brownskin ambalo alitaka DCIO Kasarani aitwe kortini kwa kudharau.
Kupitia kwa wakili wake Duncan Okatch, DJ huyo alikuwa ameomba DCIO Kasarani Jimmy Kimaru aitwe kufika kortini kwa kukiuka maagizo ya mahakama ambayo yalimtambua mbele ya mahakama ya Makadara wiki jana.

 

Hata hivyo, katika uamuzi wa Hakimu Onyina, mahakama hiyo ilisema kuwa haiwezi kuthibitisha kosa lolote la kudharau kwa kuwa maagizo ya mahakama yanayodaiwa kukiukwa yalitolewa na Mahakama ya Sheria ya Makadara ambayo ina mamlaka sawa.

 

Hakimu alibainisha kuwa Njiiri alifikishwa mbele ya mahakama yake kujibu madai ya kusaidia kujitoa uhai. Baada ya ombi hilo, wakili wake aliiomba mahakama hii kutoa wito dhidi ya DCIO Kasarani, akitaja ukiukaji wa maagizo ya mahakama.

 

Alisema wakili wa mshtakiwa alidai kuwa mteja wake alilazimishwa kukiri kosa hilo ikiwa ni sharti la kuachiliwa kwake.

 

Wakili wa upande wa mashtaka aliiambia mahakama hii kuwa masuala yaliyotolewa na upande wa utetezi yanatokana na faili tofauti zilizopo katika Mahakama ya Sheria ya Makadara hivyo ni Makadara pekee mwenye uwezo wa kushughulikia ombi hilo.

Njiiri amezuiliwa katika gereza la Industrial area.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!