Home » Abdul Nur: Wabunge Wanafaa Kuzingatia Maoni Ya Wakenya

Wabunge wana kazi ya kuhakikisha kwamba maoni ya wakenya wanawakilishwa vyema katika mswaada wa fedha 2023 unaojadiliwa katika bunge la kitaifa ndio kauli ya mchanganuzi wa masuala ya kisiasa Abdul Nur.

 

Kulingana na Nur wabunge wanafaa kuzingatia maoni ya wakenya waliochaguliwa licha ya viongozi wao wa chama kuwashinikiza kupitisha mswaada hii ikimaanisha kuwa kwa sasa huenda wakawa wafungwa wa mamlaka ya kitaifa.

 

Mswaada huo uliwasilishwa jana kwa vikao rasmi vya majdaliano ambavyo vimeanza hii leo asubuhi ili kutathimini iwapo utapitishwa au la.
Ikumbukwe viongozi mbalimbali kote nchini wamekuwa wakitoa maoni yao kuhusiana na ugumu wa maisha wengine wakipinga wengine wakiunga.

 

Aidha macho yote sasa wameelekezwa bungeni iwapo utapitishwa au kuangushwa huku muungano wa Azimio ukidokeza kwamba iwapo utapita bila shaka watandaa maandamano kote nchini kwa kuwa serikali itakuwa imeamua kutosikiza wakenya.

 

Kadhalika baadhi ya wabunge wa upinzani walipigwa marufuku ya majuma mawili wengine siku tano kwa utovu wa nidhamu kukiwepo madai ya bunge kutumia idadi kubwa ya wabunge wa Kenya kwanza kupitisha mswaada huo.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!